Hossein Amir-Abdollahian alisema hiyo jana Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Lebanon, Faisal Mekdad huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon, kikiwa ni kituo cha pili cha ziara yake ya kieneo, baada ya kuitembelea Iraq.
Amesema taarifa hiyo ya Arab League haiakisi mitazamo ya mawaziri wote wa mambo ya nje wa nchi za Kiislamu na kusisitiza kuwa, Iran, Iraq na nchi nyingine katika eneo zinaunga mkono kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislami OIC.
Mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wasio na ulinzi wa eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kwa mabavu yangali yanaendelea. Wapalestina zaidi ya 1,500 wameuawa shahidi mpaka sasa, mbali na wengine zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, huku utawala katili wa Israel ukiendelea kuwashambulia kwa mabomu na makombora Wapalestina wa Gaza.
342/